Diamond na Rayvanny washtumiwa kukopi video

0
198

Wimbo mpya wa msanii Diamond Platinumz na mwenzake rayvanny ambao umetoka hivi karibuni unadaiwa kuiga baadhi ya scene kutoka katika wimbo mwingine ambao uliwahi kutoka hapo nyuma kidogo.

Wimbo huo ambao hauna siku nyingi tangu video yake imetoka unadaiwa kutolewa baadhi ya vipande kutoka katika wimbo mmoja wapo wa hip -hop kutoka nje ya nchi.

Mashabiki wengine wamemshambulia Diamond Platinumz na kumtuhumu sana kuwa imekuwa kama kawaida ya wasanii hawa ku-copy na ku-paste nyimbo kutoka kwa wasanii wengine nje ya nchi.

Video ya wanamuziki hao imetoka jana ambapo baadhi ya mashabiki wamesema kuwa wimbo huo umeiga baadhi ya sehemu ya wimbo mwingine.

LEAVE A REPLY