Diamond na Alikiba watoswa tuzo za MTV EMA

0
65

Wanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba na Diamond Platnumz wametoswa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za MTV EMA 2018 baada ya majina yao kutokuwepo kwenye orodha ya kipengele cha Best African Act.

Alikiba na Diamond Platnumz waliwahi kushinda tuzo hiyo kupitia kwenye kipengele cha Best African Act lakini kwasasa wameshindwa kuingia kwenye kipengele hicho.

 Wasanii watakaochuana kwenye kipengele cha Best African Act ni Davido na Tiwa Savage wote kutoka Nigeria, Distruction Boyz na Shekinah kutoka Afrika Kusini na Fally Ipupa DR Congo.

Kwa upande wa Afrika Mashariki inawakilishwa na msanii Nyansiski kutoka Kenya ambaye atachuana na wasanii hao waliotoka ukanda wa Afrika Magharibi.

Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2015 huku Alikiba alishinda tuzo hiyo mwaka 2016 ambapo alichuana vikali na mkali kutoka Nigeria, Wizkid.

LEAVE A REPLY