Diamond kusaka vipaji vya watangazaji wa Wasafi Radio na Tv mikoani

0
579

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza kuzunguka mikoani kwa ajili ya kutafuta vipaji vya watangazaji wa Wasafi radio na Tv.

Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram ameuliza swali kwa baadhi ya watu kuwa mkoa gani una vipaji vya watangazaji.

Mwanamuziki huyo kwasasa amefungua radio na Tv yake kwa ajili ya kurusha matangazo ambapo hivi karibuni itaanza kurusha matangazo yake.

Wiki iyopita kupitia akaunti za meneja wake Babu Tale na Salam SK waliweka video ikionesha mafundi wakifunga mitambo kwenye radio na Tv ikihashiria mambo yanaanza kuwa mazuri.

Baada ya kukamilika Radio na Tv hiyo, Diamond atakuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Tanzania kufungua radio na Tv.

LEAVE A REPLY