Diamond aweka wazi tarehe ya Wasafi Festival

0
315

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewataka mashabiki kujitokeza kwenye Tamasha la Wasafi litakalofanyika Dar es Salaam Novemba 9 mwaka huu.

Diamond Platnumz amesema KUWA tamasha hilo litakuwa la kipekee kuwahi kufanyika Dar Es Salaam hivyo amewahimiza mashabiki wanaopenda burudani kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha hilo.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa tamasha hilo litaanza saa 1:00 asubuhi siku ya Jumamosi Novemba 9, 2019 na litamalizika saa 6:00 usiku hivyo amewataka wazazi waje na watoto wao kwenye tamasha hilo kwani kutakuwa na michezo ya watoto kabla ya kuanza burudani.

Diamond amesema kutakuwa na aina zote za muziki, kwenye tamasha hilo pia watakuwepo wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wapya na wa zamani, Muziki wa Dansi, Singeli pamoja na bendi za muziki wa taarabu.

Tamasha hilo ambalo litafanyika katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam, Huenda likahamishwa na kufanyika katika uwanja wa Taifa-Temeke endapo ombi la Diamond kwa Waziri Mwakyembe la kutumia uwanja huo litakubaliwa.

Tamasha la Wasafi Festival 2019, tayari limeshafanyika takribani mikoa 7 Tanzania bara ikiwemo Iringa, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga na Dodoma.

LEAVE A REPLY