Diamond awatoa hofu wasanii kuhusu malipo ya Wasafi Festival

0
897

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameahidi kuondoa vilio vya wasanii kuhusu malipo madogo wanayoyapata kupitia matamasha wanayofanywa hapa nchini.

Diamond amesema hayo wakati akitangaza ujio wa Tamasha la Wasafi Festival linaloandaliwa na lebo ya Wasafi.

Pia Diamond amesema kuwa wasanii wote watakaoshiriki kwenye tamasha hilo watalipwa vizuri kadri wanavyostahili.

Tamasha hilo litafanyika katika mikoa tofauti hapa nchini na mashabiki wa muziki watashuhudia wasanii tofauti kwenye tamasha hilo.

Kwa upande mwingine, Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kuwa tarehe rasmi ya kuanza kwa tamasha hilo itatangazwa baadae.

LEAVE A REPLY