Diamond awaonya wasanii watoa rushwa

0
97

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amewataka wasanii kuacha tabia ya kutoa pesa kwa ajili ya kutaka nafasi za nyimbo zao kupigwa katika Tv yake.

Diamond amesema kuwa kwa uande wake alishasema kabisa kuwa kila anaeleta nyimbo yake katika Tv hiyo basi itapigwa lakini kama kuna mtu anakuwa akitaka kutoa pesa ili aweze kupewa muda mwingi wakati kazi yake sio nzuri kuliko wengine basi huyo hana nafasi katika Tv hiyo.

Akiongea katika mkusanyiko mkubwa wa wasanii uliofanyika jana, baada ya mkuu wa mkoa kukutana na wasanii kuzungumzia changamoto za wasanii wa bongo movie na muziki.

Diamond amesema kuwa Tv yake ni ya bure kabisa na hakuna haja ya kutoa pesa hivyo kwake suala hilo hakuna kwani kila msanii ana haki sawa ya kupigwa kwenye Tv yake.

Diamond ni msanii mmoja wapo anayemiliki Tv na Radio yake ya wasafi ambapo anatoa nafasi ya kila msanii nyimbo yake kupigwa kwenye media yake bila kutoa malipo yoyote.

LEAVE A REPLY