Diamond atoa hoteli yake kusaidia wagonjwa wa Corona

0
148

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametoa ruhusa kwa Serikali kuitumia Hoteli yake mpya aliyoinunua kama hospitali ya kuhudumia wagonjwa corona.

 

Diamond amesema hayo ikiwa ni siku mbili baada kutangaza kuwalipia nyumba watu 500 ili kuondokana na adha ya kodi katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa covid-19.

 

“Misukumo ya kusaidia watu, imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia, napata moyo wa kusaidia wengine.

 

“Nimenunua hotel maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam ina vyumba zaidi ya 30, nimeshakabidhiwa documents zangu, ipo kwenye marekebisho kadhaa kisha nitaitambulisha.

 

Diamond amesema kuwa yupo radhi kuitoa hoteli kwa serikali kwa muda huu ili iweze kutumika kama Karantini au Hospital mpaka pale Corona itakapoisha.

 

Pia Diamond amesema hajaweka kiwango cha mwisho cha kodi atakazowalipia wananchi, lakini lazima ataangalia wenye uhitaji haswa.

 

Amefanya hivyo Kwa sababu wapo wanaolipa pesa kubwa mpaka Tsh million 1 kwa mwezi, na mwengine Tsh 60,000 tu na inawashinda.

LEAVE A REPLY