Diamond atinga mahakamani kwa ajili ya kesi ya matunzo ya mtoto

0
253

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz leo amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili ya kushindwa kumtunza mtoto wake aliyezaa na msanii mwenzake Hamisa Mobeto.

Shauri la kesi hiyo lililofunguliwa na Hamisa Mobetto akiomba Mahakama iamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, litaanza kusikiliza leo katika mahakama ya watoto Kisutu.

Mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Kisutu, Diamond alipitiliza na kuelekea hadi Mahakama ya Watoto iliyopo ndani ya viunga vya Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya shuri hilo.

Baada ya kutoka ndani ya Mahakama Diamond amesema kuwa aliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuweka mambo sawa kuhusu malezi ya mtoto wao.

Kwa upande wa Mobeto hakupatikana kuelezea kilichoendelea kwenye kesi hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

LEAVE A REPLY