Diamond athibitisha kumnunulia nyumba Hamisa Mobetto

0
915

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha tetesi zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa amemnunulia mjengo mma watoto wake Hamisa.

Baada ya Diamond kuachana na Zari na Kurudisha majeshi kwa Hamisa imekuwa ikisemekana kuwa Hamisa amehama alipokuwa anaishi na kuhamia kwenye mjengo mpya kabisa na mtoto wake Dylan na Fantasy.

Taarifa zilisambaa kuwa mjengo wenyewe ni ghorofa  ambalo ni bonge wa mjumba ambao upo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach.

Diamond amethibitisha taarifa baada ya kuandika Instagram na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa nyumba hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia wake kama utakumbuka ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi Lakini pia ameshamnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini South Africa.

LEAVE A REPLY