Diamond atangaza tarehe ya kufunga ndoa

0
200

Mwanamuziki wa Bongo Fleva,  Diamond Platnumz amefunguka na kutangaza kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Tanasha siku ya Februari 14 mwakani.

Kupitia mtandao Instagram, Diamond amesema harusi yake na mrembo huyo kutoka Kenya itafanyika tarehe 14 February mwakani 2019.

“Unajua ni kiasi gani naisubiria siku hiyo (siku ya harusi) father. 14/2/2019 siku ya harusi ya simba,”ameandika Diamond kwenye Instagram ambapo alimjibu mdau mmoja aliyehoji kuhusu ndoa.

Mapenzi ya wawili hao yameanza kushamili kwa miezi miwili sasa, ambapo wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Wasafi Festival mkoani Mtwara, Diamond alimtambulisha rasmi mrembo huyo .

Wawili hao kwasasa wameonekana wakiwa pamoja kila mahali kwenye Tamasha la mwanamuziki huyo lijulikanalo kama Wasafi Festival.

LEAVE A REPLY