Diamond atajwa kuwania tuzo Marekani

0
878
Diamond Platnumz

Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania Tuzo za Peoples Choice 2019 akichuana na wasanii wenzake kama vile Davido, Wizkid na Tiwa Savage.

Kwenye Tuzo hizo ambazo zinaandaliwa na Kituo cha runinga cha Nchini Marekani cha E!, Diamond Platnumz ametajwa kwenye kipengele cha “African Influencer of 2019” ambayo anachuana na Bonang Matheba, Cassper Nyovest, Davido, Minnie, Tiwa Savage, Wizkid na Yemi Alade.
.
Shawn Mendez, Post Malone, Ed Sheeran, Drake na Travis Scott pia wametajwa kwenye kipengele cha ‘Male Artist of 2019’ kwenye tuzo hizo.

Wakati Ariana Grande, Taylor Swift, Cardi B, Hasley, Billie Eillish, Miley Cyrus, Camilla Cabello na Pink wakichuana kwenye kipengele cha ‘Female Artist of 2019’. Washindi wa Tuzo hizo wanachaguliwa na mashabiki kwa mfumo Kura.

LEAVE A REPLY