Diamond ashinda tuzo ya Afrimma nchini Marekani, Davido na Wizkid chali

0
379

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo ya Afrimma baada ya kuwabwaga wanamuziki Davido na Wizkid.

Diamond amefuzu tuzo hiyo katika kipengele cha Best Artist of The Year baada ya kupata kura zaidi ya wasanii wenzake.

Utoaji wa tuzo hizo umefanyika usiku wa kuamkia leo katika jiji la  Taxes nchini Marekani ambapo wasanii kibao walihudhuria tuzo hizo.

Wasanii ambao waliokuwa kwenye kipengele hicho ni Davido, Wizkid, Diamond, Fally Ipupa, Casper Nyovest, na Tekono.

Wengine ni Eddy Kenzo kutoka Uganda, Mr Eazi kutoka nchini Nigeria na mwingine ni C4 Pedro kutoka nchini Angola.

LEAVE A REPLY