Diamond apata shavu kwenye album mpya ya Alicia Keys

0
39

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameshirikishwa kwenye album mpya ya Alicia Keys iitwayo ‘ALICIA’ inayotarajiwa kutoka rasmi Ijumaa, Septemba 18 mwaka huu.

Alicia alitangaza tarehe hiyo kuwa ataachia rasmi album yake ya saba ambapo katika orodha ya nyimbo za Album ‘ALICIA’, Alicia amemshirikisha msanii Diamond kwenye wimbo, ‘Wasted Energy’.

Album hiyo mpya ya Alicia ilipangwa kutoka rasmi mapema mwezi Machi Mwaka huu, ikahairishwa kutokana na janga la Corona.

Msanii anakuwa mwanamuziki wa kwanza kumshirikisha msanii kutoka Tanzania kwenye album yake itakayotoka hivi karibu nchini Marekani.

Wasanii wengine walioshirikishwa kwenye album hiyo ni pamoja na Jill Scott, Miguel, Khalid, Snoh Aalegra, Sampha na Ed Sheeran ambayo wamekula shavu kwenye albu.

Album hiyo itakuwa ni ya saba kwa msanii toka aanze kazi yake ya muziki hivyo mashabiki zake watarajia album bora kutoka kwa mwanamuziki huyo.

LEAVE A REPLY