Diamond aongoza orodha ya nyimbo zilizosikilizwa sana Youtube

0
30

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost orodha ya nyimbo 10 zilizotazamwa zaidi katika bara la Afrika kupitia mtandao wa YouTube kwa mwaka 2020.

Nyimbo hizo 10 wimbo namba moja ni Jeje wa Diamond Platnumz huku wimbo alioutoa wiki kadhaa nyuma WAAH aliomshirikisha Koffi Olomide ukishika nafasi ya tatu.

Kupitia Instagram yake ameandika hivi:  kwasababu ya Upendo wenu mmeniwezesha kuiwakilisha vyema Nchi yetu na kupata Most viewed song 2020, lakini pia ata kwa wimbo tulio utoa Ndani ya Muda Mfupi tu Waah kushika nafasi ya 3.

Pia ameongeza kwa kuandika Hii inaonesha ni kiasi gani Muziki wetu unazidi kukua na kusambaa duniani kote kwa ujumla.

Mwisho amemalizia kwa kuandika Nawashukuru na kuwathamini, Tuendelee kuutangaza Muziki wetu ili uzidi kutengeneza ajira, na kushiriki kukuza uchumi wa Taifa letu.

LEAVE A REPLY