Diamond amwagiwa sifa na waandaaji wa tuzo za Grammy

0
58

Waandaaji wa tuzo kubwa za muziki duniani za Grammy wamemuelezea mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuwa amebadilisha taswira ya muziki wa Afrika Mashariki kutokana na ubora wa nyimbo zake.

Waandaaji hao wamesema hayo baada ya kumfanyiwa mahojiano maalumu na waandaaji wa Tuzo kubwa duniani za Grammy.

Waandaaji wa tuzo hizo za Grammy wamemuelezea, Diamond Platnumz kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya Muziki wa Afrika Mashariki Pamoja na kufikia viwango ambavyo ni ndoto ya kila mwanamuziki kufika .

Pia wamesifu jitahada za Diamond , kuweza Kuongezea Radha za Kiingereza na Kiswahili katika Muziki wa “BongoFleva” kitu kilichofanya aweze kuvuka mipaka na kufanya kazi na Wasanii wakubwa duniani kama vile Omarion, Rick Ross, Neyo na Alicia Keys.

Tuzo za Grammys ndio Tuzo kubwa zaidi za Muziki Duniani na ndoto ya kila mwanamuziki kushinda tuzo hizo zinazoandaliwa nchini Marekani.

LEAVE A REPLY