Diamond amaliza tofauti zake na Naibu waziri, Juliana Shonza

0
337

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu wake Juliana Shonza ili kutatua tofauti zao.

Mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ofisi za Basata zilizopo maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo mazungumzo yao yalidumu kwa masaa matatu.

Katika mazungumzo hayo walizungumzia kuhusu nyimbo za Diamond kufungiwa na kuelezana ukweli kuhusu mmomonyoko wa maadili kwenye nyimbo za muziki wa Bongo Fleva.

Diamond amemhakikishia Waziri Mwakyembe kuwa atalinda maadili kwa nguvu zake zote hususani kwenye kazi zake.

Waziri Mwakyembe amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kama BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA kuitisha vikao mara kwa mara na wasanii ili kujadili masuala ya Sanaa.

Diamond Platnumz aliongozana na Mameneja wake watatu, Sallam Sharaf, Babu Tale na Said Fella.

LEAVE A REPLY