Diamond alivyombadili dini Tanasha

0
441

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa ni kweli mpenzi wake wa zamani Tanasha Donna alibadilisha dini na kuwa Muisilamu ili wafunge ndoa.

Diamond amesema kuwa ni kweli walipokuwa Kigoma Tanasha alibadili Dini Na Kuwa Muisilamu na Katika hili anamshukuru sana Ricardo Momo ambaye ndiyo mtu aliyefanikisha kwa Tanasha kubadilisha dini.

 Pia Diamond alisema kuwa alimwambia Ricardo Momo ukijitahidi Tanasha abadili dini anampa kiwanja kwahiyo Ricardo Momo likuwa Anampa Mazuri Ya Dini Ya kiisilamu.

Kutokana na mafundisho hayo baadae akasema Anaanza Kuupenda Uisilamu na baadae akabadili Dini na kuwa muislamu kabisa kwa kuapa.

Diamond na Tanasha kwasasa awapo katika mahusiano kutokana na kugombana na mwanamke huyo kwasasa yupo kwao nchini Kenya akiendelea na mambo yake huku akiwa na mtoto mmoja aliezaa na Diaomond.

LEAVE A REPLY