Diamond, Alikiba na Harmonize kuchuana kwenye tuzo za AEUSA

0
45

Wasanii wa Bongo Fleva, Alikiba, Dimaond Platnumz na Harmonize wametajwa kuwania tuzo za AEAUSA zinazoshirikisha wasanii kutoka bara la Africa.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo ni Zuchu kutoka WCB, Maua Sama, Marioo, Rayvanny, kundi la Weusi na kundi la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii Aika na Nahreal.

Wasanii hao wametajwa kuwania vipengele mbalimbali katika tuzo za AEAUSA zitakazotolewa mwishoni mwaka huu baada ya maandalizi kukamilika.

VipengeLE hivyo vilivyotawala majina ya wasanii wa bongo ni Best Male Artist, Best Female Artist, Hottest Group of the Year, Best Colaboration, Best Music Video, Entertainer of the year,.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa ifikapo Desemba 12 mwaka huu baada ya maandalizi yote kukamilika kuelekea utoaji wa tuzo hizo.

LEAVE A REPLY