Diamond, Alikiba, Harmonize na Rayvanny watajwa orodha ya wasanii 100 bora Afrika

0
56

Kituo cha Televisheni cha Burudani kutoka nchini Ghana “WatsUp TV” wametangaza orodha ya Wanamuziki 100 wa Kiafrika walio Juu zaidi kwa 2021,orodha hiyo imewajumuisha wasanii kutoka Tanzania Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize, Navy Kenzo na Rayvanny.

Orodha hiyo imekamilishwa na wanamuziki kutoka nchi 26 za Afrika ikiwa ni pamoja na Angelique Kidjo, Burna Boy, Davido, Wizkid, Mohammed Mounir, Cassper Nyovest, Khaligrapgh Jones, Sarkodie na wasanii wengine.

Orodha ina jumla ya wasanii 18 wa kike na wasanii 73 wa kiume huku makundi yakiwa 9, katika orodha hiyo msanii mdogo zaidi ni msanii kutoka Nigeria Heisrema akiwa na miaka “20” na msanii mkubwa zaidi ni msanii kutoka Misri Mounir akiwa na umri wa miaka 66.

Nigeria imeongoza kwa kutoa wasanii 26 katika orodha hiyo wakifuatiwa na Ghana wasanii 10, Ivory Coast 7 na Afrika kusini wasanii 6.

LEAVE A REPLY