Diamond akutana na watoto wake kwa mara ya kwanza

0
811

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz amekutana na watoto wake kwa mara ya kwanza toka atengane ne mpenzi wake Zari.

Diamond amekutana na watoto wake nchini Afrika Kusini ambapo watoto hao wanaishi na mama yao mzazi Zari.

Toka Diamond agombane na Zari hakuna picha iliyomuonesha akiwa na watoto wake Tiffa na Nillan.

Pamoja na kwamba mara ya kwanza alikuwa akisema amekuwa akienda kuwaona watoto wake Afrika ya kusini lakini hakukuwahi kuwa na picha iliyowahi kuthibitisha  hilo.

Jana walitoa picha hiyo kwa mara ya kwanza kwa takribani miezi minne tangu walipokuwa wamegombana.

LEAVE A REPLY