Diamond afunguka bifu lake na Alikiba

0
225
Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kukanusha kuwa na bifu na mwanamuziki mwenzake Alikiba kama inavyosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Diamond amesema kuwa kwa upande wake hana tatizo na Alikiba ila kuna baadhi ya watu wanatengeneza bifu hiyo kwa maslai yao binafsi lakini wao kama wanamuziki hawana tatizo kabisa.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa hawezi kuwa na bifu na mtu yoyote kwa kuwa hafaidiki na chochote kwenye bifu hiyo.

Diamond na Alikiba inasemekana kuwa na bifu kwa muda mrefu sana huku kila mmoja akikataa kuwa na bifu na mwenzake.

Diamond amesisitiza kuwa hawana bifu ila kuna muda watu wanakuwa wnawachochea maneno maneno ili kutaka watengeneze bifu.

Diamond amesema hawezi kuwa na tatizo na Alikiba kwani kila mtu ana mashabiki zake hivyo hana haja ya kuwa na ugomvi naye.

LEAVE A REPLY