Diamond ahudhuria uzinduzi wa Foundation ya Haji Manara

0
153

Ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amefanya uzinduzi wa pafyumu yake inayoitwa ‘De Le Boss’ sambamba na kuzindua Haji Manara Foundation aliyoianzisha kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi.

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Posta na kuhudhuriwa na mastaa wengi pamoja na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

RC Makonda amempongeza Manara kwa hatua hiyo kubwa na kisha kumuita Diamond Platnumz na mpenzi wake Tanasha mbele ya shekhe mkuu wa mkoa wa Dar, Alhad Musa Salim,  na kuwatishia kuwa angewafungisha ndoa ya mkeka.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na mastaa mbali mbali nchini akiwemo Diamond mwenyewe na mpenzi wake, Steve Nyerere, Batuli, Shilole na wengine kibao.

LEAVE A REPLY