Diamond afunguka kuhusu albam yake mpya ‘A Boy From Tandale’

0
354

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond amesema kuwa albam yake ya ‘A Boy From Tandale’ anaichukulia kama albam yake ya kwanza ingawa amewahi kutoa albam kadhaa kwa sababu imebeba lengo kubwa la kuiweka kiganjani dunia ya muziki.

Diamond amesema kuwa ndani ya albam hiyo amewashirikisha wasanii wakubwa duniani ambao watasaidia pia kuisukuma Bongo Fleva kupanda kwenye kilele cha muziki pendwa duniani.

Amesema wimbo wake na Rick Ross ambao unaitwa ‘Waka’ amechanganya Kiswahili na kiingereza kama alivyofanya kwenye kolabo nyingine.

Mbali na wasanii wa nje, amesema amewapa shavu pia wasanii wa ndani akiwemo rapa Young Killer.

Kuhusu mauzo ya albam hiyo, amesema atatumia njia za mauzo zinazotumiwa na wanamuziki wengine wakubwa kupitia mitandao husika inayofanya mauzo kimataifa.

Diamond ameenda nchini Uingereza kufanya ziara ya vyombo vya habari lakini atarejea huko mwezi ujao kwa ajili ya kufanya ‘show.

LEAVE A REPLY