Diamond afunguka kigezo anachotumia kuanzisha mahusiano ya kimapenzi

0
434

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa kigezo kikubwa anachotumia kumpata mwanamke wa kuanzisha nae mahusiano ni sura na sio tabia.

Diamond amesema kuwa mwanamke huwezi kumbadilisha sura kwa namna yoyote ile lakini tabia ni rahisi kumbadilisha.

Diamond amesema kama angetoa asilimia kwa vigezo vya sura na tabia basi asilimia 70 angetoa kwa upande wa sura na asilimia 30 zilizobaki ndio angeangalia tabia.

Pia Diamond Platnumz amefunguka kuhusu zile picha za faragha zilizovuja akiwa na Hamissa Mobetto kwa kusema kuwa walikuwa location wakirekodi kipindi cha TV.

Mwanamuziki huyo amesema kwasasa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yoyote baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Zari The Boss Lady.

 

LEAVE A REPLY