Diamond aendelea na show yake nchini Marekani

0
817

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz bado yupo nchini Marekani kwa ajili kumalizia tour ya albamu yake ‘A Boy From Tandale katika miji tofauti nchini humo.

Ni mara kadhaa kumekuwepo na stori kuwa wasanii wengi wa Afrika wanapofanya show katika nchi hiyo wengi wanaojitokeza ni wale kutoka Afrika.

Meneja kutokea WCB, Babu Tale ambaye ameongozana na Diamond katika tour hiyo, akipiga amesema kuwa show za Diamond zimekuwa ni za watu wote na si wale kutokea Afrika pekee.

Babu Tale amesema kuwa“Ukiangalia clip ambayo ameposti Diamond utaona watu weupe kibao, nimeona wazungu kibao, Jamaica walikuwepo”.

LEAVE A REPLY