Diamond achoshwa kuhusishwa na kila mwanamke

0
111

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa amechoshwa kuhusishwa kwenye mahusiano na kila mwanamke anayekuwa na urafiki naye.

Kuali ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni kuhusishwa kuingia kwenye mahusiano na mwanamke ambaye walikuwa wote nchini Dubai wakati alipokwenda kufanya shoo nchini humo wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Diamond na familia yake walionekana na mrembo mpya anayejulikana Kama Christina nchini Dubai walipokwenda kwa ajili ya shoo yake.

Diamond amesema kuwa amechoshwa na kuhusishwa na kila mwanamke anayeonekana kuwa na mama yake au kuwa naye karibu tu watu wanasema ni mtu wake.

Diamond amesema kuwa msichana huyo alikutana naye kama mwenyeji aliyekuwa akiwatembeza maeneo mbalimbali kama watu wengine ambavyo wanaweza kwenda nje na kupokelewa na marafiki zao.

LEAVE A REPLY