Deni la $2,412,283 lamtesa Nelly

0
178
NEW YORK, NY - JUNE 21: Hip-hop artist Nelly performs at Madison Square Garden on June 21, 2015 in New York City. (Photo by Brad Barket/Getty Images)

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, Nelly anadaiwa $2,412,283 ikiwa ni deni kutokana na malimbikizo ya kodi aliyokuwa akiyanya nchini humo.

Pia Nelly anadaiwa na idara ya mapato ya Missouri $149,511 za kodi kuanzia mwaka 2013.

Mashabiki wake wameendelea na mkakati wa kumsaidia rapper huyo fedha kwa kusikiliza muziki wake mtandaoni kwa kasi ya ajabu.

Usikilizwaji wa muziki wa Nelly kwenye mtandao wa Spotify umeongezeka kwa asimilia 200.

Si rahisi lakini kwakuwa mashabiki wanapaswa kusikiliza muziki wake mara 402,880,500 ili kufikisha kaisi cha $2.4m.

Wakati mashabiki wakifanya yao, sasa IRS imedaiwa kutaka kukata hela yao kupitia fedha anazopata kwenye ziara yake.

Nelly ana show nne zinazokuja ambazo IRS imewasiliana na kampuni inayokata tiketi zake show zake ili kukata fedha hizo.

Nelly ni mwanamuziki mkongwe sana nchini Marekani ambapo alipata nafasi kutamba miaka ya 2000 kutokana na nyimbo zake kutamba sana dunia kote kama nyimbo ya ‘Dilema’ ambayo alimshirikisha Kelly Rowland.

LEAVE A REPLY