DC Ilala ataka soko la Feri liwe la kimataifa

0
111

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameitaka bodi mpya ya soko la samaki (Feri) jijini Dar es Salaam kuhakikisha linageuza sura ya sasa ya soko hilo na kuwa soko la kimataifa kwa kutengenezewa miundombinu na mazingira mazuri ili kuwavutia watu wanaoingia eneo hilo.

Amesema ili soko hilo liweze kuwa la kimataifa viongozi wa soko hilo wanatakiwa kuhakikisha hakuna vibaka wanaoshinda ndani ya soko hilo na kuwataka viongozi na uongozi wa  bodi kulizungushia uzio kwa nyuma ili kuondokana na makundi maovu yanayoshinda yamekaa maeneo hayo pasipokuwa na kazi maalum.

Ameeleza kuwa  haamini kwamba soko hilo haliwezi kuondokana na harufu mbaya inayosikika eneo la Feri mtu anapokaribia eneo hilo kwani harufu hiyo inatokana na mazingira ya uchafu na  kuwataka viongozi hao kuhakikisha wanaiondoa harufu hata kwa kuweka dawa katika mazingira yanayostahili.

Aidha alifafanua kuwa si tu kwamba soko hilo linatembelewa na wakazi wa Dar es Salaam tu bali na watu kutoka mikoa mingine na mataifa ya nje kufanya utalii wao, hivyo linapaswa kuwa kivutio.

Vilevile ameitaka bodi kuhakikisha wanaongeza mapato yanayokusanywa ya kodi tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo alisema kuna wafanyabiashara takribani elfu nne hivyo mapato yanayopatikana hayaendeni na idadi kamili.

LEAVE A REPLY