DC Ally Hapi apiga marufuku siasa za uchochezi wilaya ya Kinondoni

0
217

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amepiga marufuku Wanasiasa kutoa lugha za matusi na uchochezi kwenye wilaya ya Kinondoni.

DC Hapi amesema kila mwanasiasa anayetaka kufanya siasa kwenye wilaya ya Kinondoni ni lazima achunge mdomo wake kabla ya kuongea kwa umma.

Mkuu wa wilaya huyo ametoa onyo hilo kupitia akaunti yake ya Twitter ambapo amewataka wanasiasa kufanya siasa safi na si za uchochezi.

DC Hapi ameandika “Ni marufuku siasa za matusi na uchochezi katika wilaya ya Kinondoni.Kila anayetaka kufanya siasa Kinondoni na achunge kinywa chake,”.

Kauli hiyo ya DC Hapi imekuja baada ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.

Kutokana na kauli hizo za uchochezi za Halima Mdee jana mkuu wa wilaya huyo aliagiza kukamatwa kwa mbunge huyo ambaye kwasasa anashikiliwa katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY