Dayna Nyange akanusha kutoa mimba

0
146

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amekanusha kutoa ujauzito kama habari zilivyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Dayna amesema kuwa kipindi anatoka Marekani, alikuwa na tumbo kubwa ambapo watu walidhani ni mjamzito lakini baada ya muda hakuonekana hivyo hali iliyopelekea watu kudhani ametoa ujauzito huo.

Dayna Nyange ameendelea kusema suala hilo lilifanya watu kumtuhumu kama ametoa mimba, jambo ambalo sio la ukweli japo kwa sasa ana mtoto mmoja ila hahitaji kuongeza mtoto mwingine tena.

Ameongeza kusema kuwa “Mimi ni mtoto wa Kiislam siwezi kufanya hivyo wala sitarajii na sifikirii, nina mtoto mmoja na najilinda sitaki kuwa na mwingine kwa wakati ambao nahisi sio sahihi.

Pia amesema kuwa wanasema nimetoa kwa sababu niliwahi kupost picha ambayo nilioenekana kama mjamzito kwa sababu tumbo langu lilikuwa kubwa, kwahiyo watu waliamini mimi ni mjamzito na nimetoa huo ujauzito”.

LEAVE A REPLY