Davido ashinda tuzo ya BET nchini Marekani

0
416

Mwanamuziki wa Nigeria, Davido ameshinda tuzo ya msanii Bora wa Kimataifa (The Best International Act Award) kwenye tuzo za BET zilizofanyika nchini Marekani jana usiku.

Davido amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo baada ya kuwashinda wasanii 10 kwenye kipengele hicho ambao ni Cassper Nyovest, Fally Ipupa, Tiwa Savage na Dadju kutoka nchini Ufaransa.

Wasanii wengine waliokuwepo kwenye kinyang’anyiro hicho ni Distruction Boyz, J Hus, Niska, Stefflon Don na Stormzy kutoka Uingereza.

Baada ya kushinda tuzo hiyo, Davido amewashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura za kutosha mpaka kuibuka mshindi wa tuzo hiyo.

Tuzo hizo za BET zinashirikisha wasanii wenye asili ya weusi ambazo ufanyika nchini Marekani kila mwaka.

LEAVE A REPLY