Darassa aweka wazi sababu ya kuficha mambo yake binafsi

0
726

Msanii wa Hip Hop nchini, Darassa amefunguka sababu ya kutokuweka mambo yake binasfi hadharani pamoja na kitu ambacho kinampa muonekano mzuri pindi anapokivaa.

Darassa amesema, “sina sana rangirangi, navaa kitu chochote kinachofanana na hiyo siku, kitakachofanana na mimi au kutonipa muonekano mbaya kwa mtu anayeniangalia”.

Aidha msanii huyo ameeleza sababu zinazomfanya apende kuvaa kofia kichwani ambapo amesema, “sina tatizo la kunifanya nivae kofia ndiyo nionekane mtu wa kawaida au niwe poa.

Pia amesema kuwa unaweza kuniona kwenye video nikiwa sivai kofia ila ni kitu ambacho nakuwa nacho kwenye misele yangu ya kila siku. Ni moja kati ya silaha nikiwa nayo nakuwa poa”.

Pia Darassa amesema kuwa sio lazima watu kujua mambo yake binafsi yanayohusu mama yake, mke wake au watoto wake ila wanatakiwa kuona video kali kutoka kwa Hanscana, mistari mikali kutoka kwake na midundo kutoka kwa ‘Producer’ Abbah.

LEAVE A REPLY