Darassa ashukuru mchango wa Ben Pol

0
44

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Darassa amefunguka na kusema kuwa hadi hapo alipofikia, siyo yeye, bali ni sapoti aliyopata kutoka kwa msanii mwenzake, Ben Pol.

Darasa ambaye amekuwa akisifika kuwa na staili ya kitofauti kwenye uimbaji wake, ameweka wazi kuwa, kwenye orodha ya watu wake muhimu, hawezi kumsahau Ben Pol wala kumvunjia heshima kwani anamjua vizuri katika safari yake ya muziki.

“Najua watu huwa tunasahau fadhila na mimi kiukweli nisiwe mchoyo wa kutoa shukurani, ninamshukuru sana, Ben Pol kwa mambo aliyoweza kunifanyia mpaka hapa nilipofikia.

“Alikuwa mwalimu mzuri sana kwangu na alikuwa anapenda nitimize ndoto zangu, hakutaka nisikate tamaa kabisa,” anasema Darasa.

LEAVE A REPLY