Darassa anapozikataa ‘hekima’ za Mwana FA, AY na Madee….anapotea?

2
1370

Staa wa HIP HOP ambaye kwa sasa hakuna swali shaka kuwa ngoma yake ya MUZIKI ndiyo inayo-bang zaidi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Darassa ametoka hadharani na kuipinga ‘wazi wazi’ mistari ya staa mwenzake Madee.

Miaka kadhaa ya nyuma mkongwe wa Hip Hop, Madee aliwahi kutoa ngoma na kudai biashara ya muziki wa Hip hop kwa Tanzania haina faida kabisa na ni bora kuuza pipi.

Kama hiyo haitoshi mastaa wengine wakiwemo Mwana FA na AY nao wakasitisha mpango wa kutoa albamu kwasababu muziki Bongo haulipi kwa njia ya albamu.

Lakini sasa, hit maker wa MUZIKI, Darassa amepingana na mastaa hao, yeye anaamini Hip Hop Bongo bado inalipa na albamu zinauzika na anaamini atapata anachostahiki akiachia albamu.

Pia Darassa anaamini kuwa inakuwa faraja kubwa kwa fans wake kupata mzigo uliokamilika kwenye package moja.

Je, tofauti za mitazamo hii zinaleta picha gani?

Ngoja tuone!!

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY