Darassa afungukua sababu ya ukimya wake

0
63

Msanii wa Bongo fleva aliyewahi kitikisa nchi na wimbo wake wa ‘Muziki’ Darassa amefunguka na kuweka wazi sababu iliyompelekea kukaa kimya kwa muda wa mwaka mzima.

Darassa amefunguka kuhusu ishu ya ukimya wake wa mwaka mmoja ikiwemo tuhuma zilizokuwa zikiendelea mtaani juu yake baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye game ya Bongo Fleva.

Amesema kuwa “Ni kweli nilikaa kimya sababu nilikuwa nimepata mtoto na muda wangu mwingi nilikuwa nautumia nikiwa nyumbani na hata hizo story ambazo zilikuwa zinaendelea juu yangu nilikuwa nazisikia nikiwa nyumbani kwangu’ Alisema Darassa

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa ilifika muda watu walikuwa wanakuja kugonga nyumbani kwangu ili wanione je ni kweli yanayoendelea na ikawa inafika muda nafungua geti na nawauliza vipi mnaona nini”.

Nimekaa ndani kwa mwaka mzima, wasanii wengi wametoa ngoma zao na zimefanya vizuri na nirudi rasmi kwenye muziki.

LEAVE A REPLY