Dance 100% kufikia tamati Septemba 24

0
315

Fainali ya Shindano la Dance100%  inatarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo mratibu wa shindano hilo Bhoke Egna amesema maandalizi yanaendelea vyema ambao katika shindano hilo mshindi mmoja ataibuka na kitita cha milioni 7 kama zawadi.

Bhoke amesema “Tunatarajia kufanya fainali za shindano letu Septemba 24 ambapo pamoja na kazi nzuri inayotarajiwa kuoneshwa na washiriki wetu vilevile kutakuwa na zawadi maalum kutoka kwa mashabiki watakaofika viwanjani kwa kujibu maswali na kuzawadiwa zawadi na wadhamini wa shindano Vodacom pamoja na Coca –Cola hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi’.

LEAVE A REPLY