Dame Vera Lynn aachia album akitimiza miaka 100

0
163
Dame Vera Lynn attends the 02 Silver Clef Awards at London Hilton on July 2, 2010 in London, England. (Photo by Eamonn McCormack/WireImage)

Staa wa muziki Dame Vera Lynn ameweka rekodi mpya ya muziki baada ya kuamua kusherehea umri wa miaka 100 kwa kuachia albamu mpya ya muziki.

Lynn ambaye aliweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuachia albamu akiwa na miaka 97, ameweka rekodi nyingine kwa kuachia albamu mpya akiwa na miaka 100.

Staa huyo alipata umaarufu mkubwa kwa kuwaburudisha wanajeshi wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Dame Vera ambaye atatimiza miaka 100 mwezi Machi mwaka huu ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa msanii mkubwa zaidi kuwa na albamu kwenye Top 20 za Uingereza.

Staa huyo anatarajia kuachia albamu hiyo ‘Vera Lynn 100’ mnamo tarehe 17 mwezi Machi ikiwa ni siku tat utu kabla ya kutimiza umri wa miaka 100.

vera-lynn

LEAVE A REPLY