Coutinho awasilisha ombi la kuhama Liverpool

0
179

Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho amewasilisha ombi la kutaka kuhama klabu hiyo masaa machache baada ya Liverpool kutoa taarifa kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Siku ya Jumatano, Liverpool ilikataa dau la paundi milioni 90 kutoka kwa Barcelona kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.

Mchezaji huyo ameamua kupeleka ombi hilo kutokana na uhitaji mkubwa wa mchezaji huyo ndani ya klabu ya Barcelona kwa ajili ya kwenda kuziba pengo la Neymar aliyejiunga na PSG mwishoni mwa wiki.

Coutinho ambaye ameshinda magoli 14 katika mashindano yote msimu uliopita alisaini kandarasi mpya ya miaka mitano mwezi Januari mwaka huu.

Kiungo huyo alijiunga na Liverpool mwaka 2013 akitokea klabu ya Inter Milan kwa dau la Paundi milioni 8.5.

Barcelona pia inataka kumsajili mshambuliaji wa Borrussia Dortmund, Ousmane Dembele lakini dau lao limekataliwa na klabu hiyo ya Ujerumani.

LEAVE A REPLY