Coutinho aachwa kwenye kikosi cha Liverpool dhidi ya Hoffenheim leo

0
196

Kiungo wa Liverpool, Philippe Countihno ameachwa nje ya kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki mechi ya kwanza ya michuano ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Hoffenheim leo.

Kiungo huyo wa kati, mwenye umri wa miaka 25, aliwasilisha ombi lake la uhamisho wiki iliyopita, siku chache baada ya klabu hiyo kukataa euro milioni 100 (£90m) kutoka Barcelona.

Countinho alikosa mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi katika ligi dhidi ya Watford kutokana na jeraha la mgongo.

Barca wamekuwa na matamanio ya kumpata Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa klabu ya Paris St-Germain kwa kima kilichovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 200.

Coutinho alisaini mkataba wa miaka mitano mwezi Januari, ambao haukujumuisha kipengee cha kuondoka kwake.

Liverpool wataanza kampeini yao ya Ulaya na hatua ya kwanza ya muondoano katika uwanja wa Rhein-Neckar-Arena nchini Ujerumani na mechi ya amrudiano itakuwa Anfield siku ya Jumatano tarehe 23 mwezi Agosti.

Kikosi cha Liverpool: Alexander-Arnold, Moreno, Lovren, Milner, Wijnaldum, Henderson, Can, Mane, Salah, Firmino, Kent, Solanke, Origi, Gomez, Klavan, Flanagan, Robertson, Matip, Grujic, Mignolet, Karius na Ward.

LEAVE A REPLY