Conte amwambia Costa hana mpango nae msimu ujao

0
121

Mshambuliji wa Chelsea, Diego Costa amesema ametumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa kocha Antonio Conte kuwa hana mpango nae msimu ujao.

Ndoto za Costa kubaki kwenye Uwanja wa Stamford Bride zimezimwa na kauli hiyo ya kocha ambaye hivi sasa yupo kwenye harakati za usajili kwa ajili ya kukisuka kikosi chake.

Taarifa za mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo mabingwa wa England msimu ulioisha, ziliaanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kabla hata ligi hiyo kumalizika.

Costa alikuwa anahusishwa kuhamia Ligi Kuu ya China hata hivyo hivi karibuni alibadili mawazo na kutanga kwamba angependa kuendelea kubaki England.

Nafasi yake kubaki Chelsea imekuwa ndoto kutokana na uongozi huo kuongeza kasi kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.

 

Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amepewa taarifa za kutokuwapo kwenye mipango ya Conte jambo lililomfanya kuiwa njiapanda.

LEAVE A REPLY