Clinton amnadi ‘Clinton’ Democratic

0
94

Rais wa zamani wa Marekani na mume wa mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya chama cha Democratic, Bill Clinton ameanza kumpigia kampeni mke wake Hillary Clinton baada ya kuidhinihswa rasmi na wajumbe wa mkutano mkuu kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Bill ambaye amemuelezea mke wake kama ‘rafiki mkubwa’ na ‘mfanya mabadiliko’ amewahamasisha wanachama na wanachi wa Marekani kumpa nafasi ya kuliongoza taifa hilo Bi. Hillary.

Kwenye ujumbe wake kwa wapiga kura wa Marekani, Hillary Clinton alijinasibu kuwa atakuwa rais wa kwanza mwanamke Marekani na msichana yeyote ambaye amechelewa kulala kwa kufuatilia mkutano wa Democratic basi ajue kuwa mmoja kati ya wasichana hao siku moja atakuwa mwanamke wa oili kuwa rais wa Marekani.

Clinton amewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kabla ya kuenguliwa kwenye nafasi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya.

Hata hivyo chama cha Democratic kinaonekana kuwa na msuguano huku wafuasi wa Seneta, Bernie Sanders wakionyesha wazi kutoridhishwa na Hillary Clinton kuwa mgombea kwa tiketi ya chama hicho.

LEAVE A REPLY