Chuchu Hansy awachana wasanii wenzake

0
12

Muigizaji wa Bongo Movie, Chuchu Hans amewaponda mastaa wenzake wanaozindua miradi mbalimbali ikiwemo maduka na saloon wakijifanya miradi yao kumbe si kweli isipokuwa wanataka kuipa ustaa miraji hiyo.

Chuchu alisema utasikia mara staa fulani kazindua duka lake la viatu maeneo fulani mara mwingine kazindua saloon yake eneo fulani lakini baada ya muda unakuja kugundua kumbe hakuna lolote.

Amesema kuwa “Utasikia fulani kazindua duka la viatu maeneo fulani mara mwingine kafungua saluni ya kisasa maeneo fulani tena wakitaja mpaka thamani ya hiyo miradi lakini baada ya muda unakuja kugundua kumbe hiyo ilikuwa ni kuipa kiki miradi hiyo.

Pia amesema kuwa “Mimi nimeamua kuiboresha saloon yangu hapa Sinza White Inn na nnaposema saluni yangu namaanisha yangu na sio kujipazia kwa ajili ya kuipa ustaa mimi siyo kama hao,”.

Mugizaji huyo kwa upande amesema kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kwani ana miradi yake mingi ya kufanya ili kujiongezea kipato nje ya uigizaji.

LEAVE A REPLY