Christian Bella kufanya kolabo na Werrason

0
190

Mwanamuziki wa dansi nchini, Christian Bella amesema kuwa mwanamuziki nyota wa Kongo, Werrason amekubali kufanya nae kazi baada ya kukubali uwezo wake wa kuimba.

Werrason ambaye yupo nchini kwa ajili ya shoo zake mbili naye kwa upande wake amethibitisha kufanya kazi na Christian Bella.

Werrason amesema hayo alipokutana na msanii Christian Bella na kuonyesha hisia zake juu ya msanii huyo.

Christian Bella ameliona ni jambo kubwa sana katika muziki wake kuona watu ambao alikuwa akiwasikiliza toka wakiwa wadogo saizi wanakubali kazi zake na kukubali kufanya kazi pamoja na yeye.

Christian Bella kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Niende wapi’ ambao amemshirikisha rapa Joh Makini kutoka katika kampuni ya Weusi. Itazame hapa kazi yake mpya.

LEAVE A REPLY