Chin Bees kuwainua wasanii wa trap

0
22

Mwanamuziki wa Trap Bongo, Chin Bees amesema kuwa kupitia kampuni yake ya Bees Gang Entertainment (BGE) inampango wa kuwaongezea maarifa wasanii wote wachanga kuhusu game ya Trap.

Bees amesema kuwa moja ya kusudio la BGE ni kuona namna gani inakuza uelewa wa Trap na kuufanya kuwa muziki wa biashara.

Baada rapper TI kuingia makubaliano na Chuo Kikuu cha Clark Atlanta cha  nchini Marekani kwa ajili yakufundisha kozi ya biashara ya muziki wa Trap.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa endapo Bongo itakuwa rahisi basi hatasita kushirikiana na vyuo kutoa Elimu ili kuukuza zaidi muziki wa Trap.

LEAVE A REPLY