Chid Benz: Mpinzani wangu alikuwa Ngwea

0
83

Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva nchini Chid Benz amefunguka na kusema kuwa katika maisha ya usanii kila msanii anakuwa na wimbo wake ambao unakuwa mkubwa sana kuliko nyingine.

Kauli hiyo ameitoa siku chache baada ya kuulizwa wimbo gani kwa upande wake ndiyo mkali sana amejibu na kusema wimbo wake bora wakati wote ni Dar es Salaam Stand Up.

Chid amesema kuwa pamoja na hayo kwa upand wae anaamini kuwa ngoma ambayo ilimfanya kukaa na kutambulika sana katika gemu ni ngoma ya Dar es salaam stand up ambao ulimfanya kupata mashabiki wengi sana,

Pia Chid anasema kuwa kwa anavyoamini yeye , hakuna msanii mwingine anaweza kulinganishwa na yeye zaidi ya marehemu Ngwea ambae alikuwa anaona kuwa ndie aliekuwa akimkimbiza sana katika game la muziki kipindi hicho na hakuna mwingine anaweza kutokea.

Mwanamuziki huyo kwasasa amerudi rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kuachia kibao chake kikali alichofanya na Q Chillah.

LEAVE A REPLY