Chid Benz kuachia albam mpya

0
103

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chid Benz amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuachia albam yake mpya baada ya muda mrefu kutotoa albam.

Kauli ya Chid Benz inakuja baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘King Of The Jungle (DSM)” na kusema kuwa huo ni moja kati ya wimbo uliopo kwenye Album yake anayotaka kuiachia hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Chid amepost kipande cha wimbo huo na kuandika hivi “Ahsanteni Boomplay Music na Boombuzz kwa support ya single yangu ya kwanza hio ya my new album inayotoka karibu ‘King Of The Jungle (DSM)”.

Narudi kutawala jiji langu na sauti inayo tambaa kutoka ilala kufikia Pembezoni zote za jiji mpaka dunia. Nashukuru mungu kwa kunipa uzima huu. Nenda Boomplay kasikilize Goma.”

LEAVE A REPLY