Chid Benz awataka mashabiki wasimpuuze

0
104

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz amewataka watu kumsikiliza anayosema bila kumuhukumu kwa udhaifu wake.

Chid Benz amesema kwamba mara nyingi amekuwa akiongea mambo ya msingi, lakini watu wamekuwa wakimpuuza na kumchukulia kama mtu aliyedata, huku vijana wengine wakiendelea kupotea.

Chid Benz ameendelea kusema kwamba hata kama wanamuhukumu kutumia madawa ya kulevya, lakini wasiangalie madawa anayotumia wala udhaifu mwingine, bali wachukue maneno anayoyazungumza ili kuokoa wengine.

Chid Benz amekuwa akisema mambo mbali mbali kuwasema wasanii wenzake, jambo ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakimdhihaki kutokana na uraibu ambao alikuwa nao miaka ya hivi karibuni.

Mwanamuziki huyo pia aliwahi kusema tayari amefanya collaboration na 2pac ambaye kwasasa ni marehemu jambo ambalo siyo la kawaida.

LEAVE A REPLY