Chid Benz avutiwa na kiki za wasanii

0
34

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Chidi Benz amesema anashangaa kuona watu wanaohoji kuhusu matukio ya kiki kwa sababu ulimwengu mzima ndiyo unaelekea huko kutokana na uwepo na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Chid Benz amesema kuwa “Sijaelewa kwanini watu hawataki kiki na wanajua kabisa tupo wakati wa kiki, twende mbele turudi nyuma Ulimwengu wa sasa ni kiki.

Chid amesema kuwa mitandao haiwezi kuwa mingi halafu kusiwe na kiki, inapoteza kwa sababu watu wengine wanaangalia zaidi kuliko kazi”.

“Watu wasilazimishe kusema kiki inaua au inazingua, kama unasema inazingua achana na mitandao kama Facebook, Instagram na Twitter maana ndiyo inafanya mitandao inauza kwa kupata likes nyingi na views wengi.

Mwanamuziki huyo amefunguka hayo baada ya kuwepo kwa baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva, kufanya kiki ili kuvusha muziki wao.

 

LEAVE A REPLY