Chid Benz amtaka Nay wa Mitego kubadili aina ya muziki wake

0
245

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Chid Benz amemtaka Nay wa Mitego kubadilika na kuachana na aina ya muziki anaofanya kwasasa.

Chid Benz amesema kuwa Nay anatakiwa kuachana na muziki wake wa kuwaimba wanamuziki wenzake kwa kuwakashifu na badala yake aimbe nyimbo za kuelimisha jamii.

Kauli hiyo ya Chid Benz inakuja kufuatia kuulizwa aina ya muziki anaofanya Nay wa Mitego kweli unastaili kwa jamii.

Pia Chid Benz amesema kuwa mwanamuziki huyo anatakiwa kuachia wanamuziki vijana kama vile Billnass kwani sasa ndiyo muda wao na siyo kukaa na kuanza kuwadis wasanii wenzake.

Kwa upande mwingine Chidi Benz amemtaka Nay wa Mitego kuachana na muziki kama amechoka aige nyayo za Afande Sele na Juma Nature ambao enzi zao walitamba sana kwenye muziki huo.

LEAVE A REPLY