Chid Benz afungukia upendo wake kwa baba yake

0
31

Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Chid Benz amefunguka kuhusu upendo alionao kwa baba yake ambapo amesema hata akimfanyia kosa gani kwakwe yeye haoni kama ni kosa.

Chid Benz ameeleza kuwa hakuwahi kukaa karibu sana na mzazi wake wa kiume ila hiyo haimaanishi kutokumjali kama baba.

“Uwepo wa baba yangu kwangu sioni kosa kabisa natamani nipate kingi nimgawie kidogo sioni kama anastahili adhabu yoyote hata kama alimzingua mama”. amesema Chidi Benzi

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Tunaonga kichizi huwezi kushindwa kumhudumia mzazi wako hakuna ulazima wa kumchukia baba hata kama kafanya chochote kile ,wapo watu wenye matatizo na baba zao ila nawashauri tu kwa mtoto wa kiume haijalishi kafanya nini baba yako mpende tu ni mzazi wako”.

LEAVE A REPLY